Hazina-Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Msajili wa Hazina, Waheed Muhammad Ibrahim Sanya leo tarehe 13/03/2025 alikuwa na kikao cha pamoja na viongozi wa CEOs Forum Tanzania Bara.

March 14, 2025

Msajili wa Hazina, Waheed Muhammad Ibrahim Sanya leo tarehe 13/03/2025 alikuwa na kikao cha pamoja na viongozi wa CEOs Forum Tanzania Bara. CEOs Forum ni jumuiya inayowakutanisha watendaji wa wakuu wa mashirika ya umma Tanzania Bara kwa lengo la kuzungumza mafanikio na changamoto zinajitokeza katika Taasisi zao ili kushauriana kwa pamoja nini cha kufanya katika kufikia malengo ya Mashirika hayo na kuleta maendeleo kwa nchi.

Hivyo, Msajili alikutana na viongozi hao kwa lengo la kupata uzoefu wa CEOs Forum ili Wakuu wa Mashirika ya Umma Zanzibar wawe na chombo kama hicho chenye lengo la kutatua changamoto zinazokuwa kikwazo ikiwa watendaji hao hawana sehemu ya kukutana na kuzungumza lugha mojo.
Kikao hicho kilifanyika Dar es Salaam katika Ofisi za PSSSF. Aidha, katika kikao hicho mbali ya kuhudhuriwa na watendaji wakuu wa CEOs Forum, pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa ZEEA, Maafisa waandamizi kutoka Ofisi ya Msajili Zanzibar na wenyeji Mwakilishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Tanzania Bara.

Baada ya majadiliano yaliyolenga kuanzisha CEOs Forum Zanzibar, kikao kiliazimia kufanya taratibu zote za kuwa na hio Forum kisheria lakini wanaweza kuanza kwa kuwakutanisha Watendaji wakuu ili walijue hili na walibebe kwa nguvu zote huku Msajili wa Hazina Zanzibar akibakia kiwa mlezi na mshauri.