TAARIFA KWA UMMA

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar, inapenda kuutangazia umma kuwa, Kampuni ya Uunganishaji na Usambazaji Maudhui Zanzibar (ZMUX) imefutwa rasmi kuanzia tarehe 22/09/2025. Ufutaji wa Kampuni hiyo umefanyika kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Makampuni, Nam. 15 ya 2013. Majukumu yote yaliyokuwa yakifanywa na Kampuni hiyo, yatafanywa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).