VITENGO
Muundo ulioidhinishwa wa Ofisi ya Msajili wa Hazina una jumla ya viteng vitano (5) vinavyojitegemea.
5.Kitengo cha Uhasibu na Fedha:
Majukumu ya Kitengo
1) Kuandaa na kufanya malipo ya matumizi mbali mbali ya Ofisi.
2) Kutoa ushauri kuhusiana na mambo yote ya fedha za Ofisi kwa mujibu
sheria na kanuni za fedha.
3) Kutunza kumbukumbu ya hesabu za Ofisi.
4) Kuandaa malipo na kuwasilisha katika mifuko na mikato maalum ya
watumishi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazohusika.
5) Kufuatilia upatikanaji wa fedha zilizotengwa.
6) Kufanya usuluhisho wa hesabu za Ofisi “Bank
Reconciliation”.
7) Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za kitengo.