VITENGO
Muundo ulioidhinishwa wa Ofisi ya Msajili wa Hazina una jumla ya viteng vitano (5) vinavyojitegemea.
2.Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na
Uhusiano:
Majukumu ya Kitengo
1) Kufanya uchambuzi na kubuni mifumo ya TEHAMA ya Ofisi ya Msajili wa Hazina.
2) Kuiwezesha Ofisi kutumia mifumo mingine inayoandaliwa na kutolewa kwa nia ya kurahisisha utendaji kazi.
3) Kuandaa na kutekeleza Mkakati wa TEHAMA na kuufanyia tathmini 4) Kufanya ufuatiliaji kuhusu utekelezaji wa Sera ya TEHAMA.
5) Kutunza, kutoa ushauri na kuratibu ununuzi wa vifaa vya TEHAMA
pamoja na programu (software) na “hardware”.
6) Kuanzisha, kuratibu na kuelekeza matumizi ya barua pepe katika Ofisi
7) Kuandaa na kutunza „web-portal‟ na mtandao wa Afisi.
8) Kufanya marekebisho na kusimamia matumizi ya mfumo wa usalama wa
vifaa na mifumo ya TEHAMA.
9) Kuchunguza, kutambua na kupendekeza kwa Afisi vifaa na mifumo ya
TEHAMA inayofaa na inayoweza kutumika katika Afisi.
10) Kuanzisha na kutoa mafunzo kwa watumishi juu ya utumiaji wa mifumo
na vifaa vya TEHAMA.
11) Kukuza na kujenga uhusiano mwema kati ya Ofisi ya Msajili na Taasisi
nyengine.
12) Kupokea malalamiko kutoka kwa wadau juu ya utendaji wa Ofisi ya
Msajili wa Hazina
13) Kuratibu ziara za wageni na viongozi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
14) Kuwezesha utoaji wa elimu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa wafanyakazi
na umma