Hazina-Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina

Kwa mujibu wa kifungu cha 6(a-j) cha Sheria Nambari 6 ya mwaka 2021 ya Ofisi ya Msajili wa Hazina inatekeleza majukumu

Majukumu:-

1. Kusimamia uwekezaji wa umma kwa niaba ya Serikali

2. Kuidhinisha mapendekezo ya uwekezaji wa Taasisi za Uwekezaji za Umma

3. Kusimamia na kutathmini utendaji wa jumla wa Taasisi za Uwekezaji za Umma

4. Kukuza maadili ya utawala bora katika miamala yote ya biashara, ikijumuisha utoaji wa miongozo kwa Taasisi za Uwekezaji za Umma

5. Kusimamia, kufuatilia na kutekeleza taratibu za kuundwa upya kwa Taasisi za Uwekezaji za Umma

6. Kumshauri Mheshimiwa Waziri kuhusiana na gawio

7. Kutoa miongozo na taratibu za uendeshaji kwa ajili ya usimamizi wa Taasisi za Uwekezaji za Umma

8. Kushughulikia mikataba ya utendaji na Wenyeviti, au watendaji waandamizi wa Taasisi za Uwekezaji za Umma

9. Kupitia mapendekezo ya miundo ya Taasisi na mishahara, miundo ya utumishi na motisha za Taasisi za Uwekezaji za Umma kabla ya kuwasilisha kwenye Kamisheni ya Utumishi wa Umma

10. Kupitia na kutoa mapendekezo kuhusu sera maalum na sheria zinazohusiana na uendelezaji wa Taasisi za Uwekezaji za Umma