Majukumu yake:
1) Kushughulikia masuala yote ya kiutumishi ikiwemo ajira, mishahara,
likizo, mafunzo, upimaji utendaji kazi na upandishwaji cheo.
2) Kushughulikia malalamiko, migogoro na matatizo ya wafanyakazi.
3) Kusimamia utayarishaji wa stahiki zote za wafanyakazi wa Ofisi.
4) Kusimamia utunzaji na uhifadhi wa nyaraka, faili na kumbukumbu za
wafanyakazi na Ofisi.
5) Kutayarisha mishahara na maslahi mbali mbali ya wafanyakazi.
6) Kutunza kumbu kumbu watumishi.
7) Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika
makundi kulingana na somo husika (classification and Boxing).
8) Kukusanya takwimu na kutunza kumbukumbu zinazohusu mipango ya watumishi.
9) Kuandaa mikakati na mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi.
10) Kushughulikia nidhamu kwa wafanyakazi.
11) Kushughulikia mahudhurio ya wafanyakazi.
12) Kushughulikia masuala ya usafiri.
13) Kukadiria upatikanaji wa mahitaji, vifaa na vitendea kazi na kuhakikisha vinatunzwa na kutumika ipasavyo.
14) Kusimamia huduma za masjala za utunzaji wa kumbukumbu za ofisi, uhudumu na usambazaji wa barua nyaraka, vifurushi na nyaraka za Ofisi
15) Kuandaa Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Clients Service Charter) wa Ofisi.
16) Kushughulikia masuala ya usafi wa jengo la afisi, usafiri kutunza mali za ofisi na huduma nyenginezo