Majukumu yake:
1) Kufanya usajili wa Mali za Umma zilizopo katika Taasisi za Umma.
2) Kutunza nyaraka mbali mbali za mali za Serikali.
3) Kupitia na kutoa mapendekezo kuhusu sera maalum na Sheria zinazohusiana na usimamizi na uendeshaji wa Mali za Umma
4) Kutoa taarifa kwa taasisi za umma juu ya kuwasilisha mali zinazotakiwa kuondoshwa.
5) Kuandaa na kusimamia mfumo wa usimamizi wa vyombo vya moto vya serikali kwa ajili ya kuhakikisha matumizi bora ya vyombo hivyo.
6) Kuandaa na kupitia sera za usimamizi wa mali za umma, miongozo, taratibu na maelekezo mbali mbali kwa ajili ya ufanisi wa usimamizi wa mali za umma.
7) Kudhibiti na Kuhifadhi daftari la kielektroniki la kumbukumbu za Mali zote za Umma.
8) Kuidhinisha uimarishaji wa daftari la mali ili kuhakikisha linafuata sera, sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa.
9) Kufanya ukaguzi wa Mali za Serikali katika taasisi za Umma.
10) Kusajili na kufanya uhakiki wa Mali za umma zilizopo katika Taasisi mbali mbali za Serikali.
11) Kusimamia mifumo ya uwekaji wa Kumbukumbu za Mali za Serikali.
12) Kuandaa Miongozo juu ya usimamizi na utunzaji wa Mali za Serikali