Hazina-Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Majukumu yake:

1) Kuandaa mpango mkakati, bajeti na mpangokazi wa Ofisi na kutayarisha viashiria vya utekelezaji wa mpango mkakati wa Ofisi;
2) Kuandaa ripoti za robo mwaka, nusu mwaka mwaka na kama itakavyohitajika kuhusu utendaji kazi wa Ofisi;
3) Kuratibu na kufanya tafiti za uwekezaji na usimamizi wa mali zinazohusiana na majukumu ya Ofisi ya Msajili.
4) Kuandaa mikakati na vipaumbele vya utafiti kuhusu uwekezaji na uimarishaji wa mazingira ya biashara;
5) Kutoa ripoti za tafiti za uwekezaji na usimamizi wa mali zinazohusiana na majukumu ya Ofisi ya Msajili.
6) Kukusanya taarifa na kutayarisha mpango kazi wa mwaka pamoja na mpango mkakati kwa muda wa kati wa Ofisi.
7) Kusimamia ukusanyaji, uchambuzi na usambazaji wa takwimu za Ofisi.
8) Kutayarisha mfumo wa muundo wa ukusanyaji wa taarifa na ripoti za utekelezaji.
9) Kuandaa na kuendeleza Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Ofisi