Majukumu yake:
1) Kutoa taarifa kwa taasisi za umma juu ya kuwasilisha mali zinazotakiwakuondoshwa.
2) Kufanya tathmini ya thamani za mali za Umma zinahitajika kuondoshwa katika taasisi husika.
3) Kuandaa taarifa za tathmini za mali za Umma kwa ajili ya kuwasilishwa kwa Mthamini Mkuu kwa hatua nyengine.
4) Kukusanya na kuorodhesha Mali zilizoharibika kutoka katika Taasisi za Umma ili zifutwe kwenye daftari la mali za Umma.
5) Kufanya Uthamini na uhakiki wa Mali zinazotaka kuondoshwa kutoka kwenye daftari la Mali za Serikali
6) Kuhakikisha Mali za umma zinaondoshwa kwa mujibu wa sera, sharia, kanuni na miongozo iliyowekwa.
7) Kutoa muongozo wa uondoaji Mali za Umma.
8) Kusimamia uuzaji wa mali za umma na kuweka control number za uuzaji wa mali za umma.
9) Kuhakikisha fedha zinazotokana na uuzaji wa mali za umma zinaingia katika mfuko mkuu wa Serikali.
10) Kufanya tathmini ya Mali zinazoingizwa kwenye Daftari la mali za Serikali.