Majukumu yake:
1) Kutayarisha na kuanisha Taasisi za uwekezaji katika madaraja mbalimbali.
2) Kupendekeza mgao wa faida ya mwaka, kutangaza mgao au mchango wa Taasisi za uwekezaji wa Umma.
3) Kuandaa na kusimamia daftari la Taasisi za uwekezaji za umma.
4) Kufanya uchambuzi na tathmini ya miradi mipya inayowasilishwa na Taasisi za uwekezaji wa Umma kwa dhumuni la upatikanaji wa fedha.
5) Kushauri juu ya matumizi ya fedha yasiyokuwa na tija kwa taasisi za uwekezaji.
6) Kufanya na kutoa tathmini za kiutendaji kwa taasisi zenye mitaji ya ummana uwekezaji.
7) Kupokea na kuchambua bajeti, mpango mkakati, mipango ya biashara na kutowa miongozo kwa Taasisi za uwekezaji.
8) Kutoa maoni, ushauri na mapendekezo juu ya kuzisaidia taasisi za uwekezaji wa umma kutoka kwenye vikwazo na hatua sahihi zinazopaswa kuchukuliwa.
9) Kufanya tathmini ya mwenendo wa biashara kwa taasisi za uwekezaji wa umma.
10) Kupitia na kuchambua masuala ya fedha katika taasisi za uwekezaji wa umma na kushauri ipasavyo.
11) Kufanya ukaguzi wa kuangalia mapato na matumizi katika taasisi zauwekezaji wa umma.