Hazina-Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Majukumu yake:

1) Kupitia kuchambua na kutoa mapendekezo ya miundo ya utumishi kutoka katika taasisi zilizochini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kabla ya uwasilishwa Kamisheni.
2) Kupitia na kupendekeza masuala ya mishahara na maslahi ya taasisi, wenyeviti, wajumbe wa bodi, watendaji Wakuu wa Taasisi na watumishi kabla ya kuwasilisha Serikalini
3) Kufuatilia utendaji wa wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za uwekezaji na taasisi zisizo za kibiashara zenye mitaji ya umma.
4) Kuandaa mikataba na kuweka vigezo vya ya kiutendaji kwa wenyeviti na wakuu wa taasisi zilizo chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina
5) Kutoa maoni na mapendekezo ya juu ya kanuni za ndani za taasisi za uendeshaji na usimamizi wa watumishi kabla ya kuanza kutumika.
6) Kupendekeza njia bora na mifumo ya uendelezaji na usimamizi wa utumishi wa mashirika na taasisi zisizo za kibiashara
7) Kupitia Mapandekezo ya Muundo wa Taasisi kabla ya kuwasilishwa Kamisheni ya Utumishi.
8) Kutoa ushauri na mapendekezo ya uanzishwaji wa taasisi mbali mbali zinazohusiana na uwekezaji na zisizo za uwekezaji.