Hazina-Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Muundo una idara tatu (3) ambazo ni Idara ya Mitaji ya Umma na Uwekezaji, Idara ya Usimamizi na Usajili wa Mali za Umma, Idara ya Rasilimali Watu, Utawala na Mipango na Ofisi ya Msajili wa Hazina Pemba.

1. Idara ya Rasilimali Watu, Utawala na Mipango

Idara hii ina divisheni tatu (3) ambazo ni Divisheni ya Rasilimali Watu na Utawala, Divisheni ya Mipango na Utafiti na Divisheni ya Utunzaji Kumbukumbu.

Majukumu yake:

1) Kusimamia matumizi ya mali za Ofisi ya Msajili ikiwemo vyombo vya
usafiri, mitambo, samani, vifaa vya kuandikia na vifaa vya mawasiliano,
2) Kusimamia shughuli za masjala ya siri na dhahiri.
3) Kutafsiri na kushughulikia utekelezaji wa Miundo ya Utumishi na Miundo
ya Taasisi, pamoja na mifumo mengine ya kiutumishi na uendeshaji.
4) Kusimamia masuala ya ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo kwa
Watumishi.
5) Kuhakikisha kuwepo kwa watendaji wa kutosha na wenye sifa na kuweka
kumbukumu za masuala yanayohusu watendaji.
6) Kusimamia kumbukumbu za Ofisi.
7) Kuratibu masuala Mtambuka yakiwemo (UKIMWI, jinsia, mabadiliko ya
tabianchi; walemavu na mengineyo).
8) Kuratibu/kutoa huduma za ulipaji wa mishahara, maposho, mikopo na
matayarisho ya mafao ya uzeeni;
9) Kusimamia matengenezo ya jengo, vyombo vya usafiri.
10) Kuandaa, kuhuisha na kusimamia utekelezaji wa mkataba wa utoaji wa
huduma;
11) Kuratibu na kuandaa ikama, utekelezaji wa mipango ya rasilimaliwatu na
Urithishwaji wa madaraka;
12) Kutunza kumbukumbu za watumishi;
13) Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo na kuandaa mipango ya
mafunzo.
14) Kusimamia nidhamu na maadili ya watumishi;
15) Kutafsiri na kusimamia sheria, kanuni na miongozo ya kazi.
16) Kuratibu utekelezaji wa upimaji utendaji kazi.