IMuundo una idara tatu (3) ambazo ni Idara ya Mitaji ya Umma na Uwekezaji, Idara ya Usimamizi na Usajili wa Mali za Umma, Idara ya Rasilimali Watu, Utawala na Mipango na Ofisi ya Msajili wa Hazina Pemba.
2. Idara ya Mitaji ya Umma na Uwekezaji
Idara hii ina divisheni mbili (2) ambazo ni Divisheni ya Usimamizi na Usajiliwa Mali za Umma na Divisheni ya Uondoaji wa Mali za Umma.
Majukumu yake:
1) Kupitia na kutoa mapendekezo kuhusu sera maalum na Sheria
zinazohusiana na usimamizi na uondoaji wa Mali za Umma
2) Kutoa taarifa kwa taasisi za umma juu ya kuwasilisha mali zinazotakiwa
kuondoshwa.
3) Kufanya tathmini ya mali za Umma zinahitajika kuondoshwa katika
taasisi husika.
4) Kuandaa taarifa za tathmini za mali za Umma kwa ajili ya kuwasilishwa
kwa Mthamini Mkuu kwa hatua nyengine.
5) Kuandaa na kusimamia mfumo wa uekaji wa kumbukumbu wa mali za
umma nakuweka alama za utambuzi wa mali za umma.
6) Kutunza nyaraka mbali mbali za mali za Serikali.
7) Kuandaa na kusimamia mfumo wa usimamizi wa vyombo vya moto vya
serikali kwa ajili ya kuhakikisha matumizi bora ya vyombo hivyo.
8) Kusimamia uuzaji wa mali za umma na kuweka control number za uuzaji
wa mali za umma.
9) Kuhakikisha fedha zinazotokana na uuzaji wa mali za umma zinaingia
katika mfuko mkuu wa Serikali.
10) Kuandaa na kupitia sera za usimamizi wa mali za umma, miongozo,
taratibu na maelekezo mbali mbali kwa ajili ya ufanisi wa usimamizi wa
mali za umma.
11) Kudhibiti na kuhifadhi daftari la kielektroniki la kumbukumbu za Mali
zote za Umma.
12) Kuidhinisha uimarishaji wa daftari la mali ili kuhakikisha linafuata sera,
sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa.
13) Kufanya ukaguzi wa mali katika taasisi za Umma kwa mujibu wa mahitaji.
14) Kuhakikisha kwamba muundo unaohusiana na mali za umma unawekwa
kwa mujibu wa viwango vinavyokubalika
15) Kuhakikisha Mali za umma zinaondoshwa kwa mujibu wa sera, sheria,
kanuni na miongozo iliyowekwa.
16) Kukusanya na kuorodhesha Mali zilizoharibika kutoka katika Taasisi za
Umma ili zifutwe kwenye daftari la mali za Umma.