Hazina-Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Muundo una idara tatu (3) ambazo ni Idara ya Mitaji ya Umma na Uwekezaji, Idara ya Usimamizi na Usajili wa Mali za Umma, Idara ya Rasilimali Watu, Utawala na Mipango na Ofisi ya Msajili wa Hazina Pemba.

3. Idara ya Mitaji ya Umma na Uwekezaji

Idara hii ina divisheni mbili (2) ambazo ni Divisheni ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma na Divisheni ya Usimamizi wa Mifumo ya Kiutawala na Maslahi

Majukumu yake:

1) Kutayarisha miongozo mbali mbali inayohusiana na usimamizi wa
taasisi za uwekezaji na zenye mitaji ya umma.
2) Kuandaa mikataba ya kiutendaji na viongozi Wakuu wa Taasisi za
uwekezaji na Taasisi zenye mitaji ya Umma
3) Kushauri juu ya namna bora ya kuongeza mitaji ya katika mashirika ya
umma
4) Kusimamia uwekezaji wa umma kwa niaba ya Serikali
Kuidhinisha mapendekezo ya uwekezaji wa Taasisi za Umma
5) Kufanya uchambuzi wa bajeti za Mashirika na taasisi zenye mitaji ya
umma.
6) Kuandaa miongozo kuhusiana na utoaji wa gawio na uwasilishaji wa
michango katika mfuko mkuu wa serikali
7) Kusimamia utendaji wa wenyeviti, wajumbe wa Bodi na watendaji wakuu
wa taasisi zinazosimamiwa na Msajili.
8) Kutoa maoni na mapendekezo ya miundo ya taasisi na miundo ya
utumishi ya mashirika ya umma, Taasisi zenye mitaji ya umma
zinazosimamiwa na Msajili kabla ya kuwasilishwa Kamisheni
9) Kutoa maoni na mapendekezo kuhusu ulipaji wa maslahi na motisha
mbali mbali kwa taasisi zenye uwekezaji na zinazosimamiwa na Msajili.
10) Kupitia na kutoa maoni, ushauri na mapendekezo juu ya miradi
mipya/uwekezaji kwa lengo la kukuza mitaji ya umma.
11) Kuandaa na kuingia mikataba ya kiutendaji na viongozi wakuu wa
taasisi za uwekezaji na taasisi zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili
12) Kutoa miongozo kuhusiana na bajet, mipango mkakati na kibiashara na
mambo mengine yanayohusiana nayo katika taasisi zinasimamiwa na
Ofisi ya Msajili
13) Kushauri namna bora za matumizi ya fedha katika taasisi za umma kwa
lengo la kupunguza matumizi

14) Kufuatilia utekelezaji wa taratibu za kuundwa upya kwa taasisi za
uwekezaji na zilizo chini ya Msajili
15) Kufanya ufuatiliaji wa miradi na masuala mbali mbali yanayohusiana na
uwekezaji na mitaji ya umma.