Hazina-Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

TAARIFA KWA UMMA

October 9, 2025

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar, inapenda kuutangazia umma kuwa, Kampuni ya Uunganishaji na Usambazaji Maudhui Zanzibar (ZMUX) imefutwa rasmi kuanzia tarehe 22/09/2025.

Ufutaji wa Kampuni hiyo umefanyika kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Makampuni, Nam. 15 ya 2013.

Majukumu yote yaliyokuwa yakifanywa na Kampuni hiyo, yatafanywa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).