
Kwa niaba ya Msajili wa Hazina, Ndugu Khadija Masoud Haji Mkurugenzi Utumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina akipokea Tunzo ya shukrani kutoka kwa Uongozi wa Taasisi ya Wataalamu wa Udhibiti wa Udanganyifu katika Kongamano la Kimataifa la Mapambano dhidi ya Udanganyifu katika Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki. Kongamano hilo limeanza Tarehe 24-28 Februari, 2025 katika Ukumbi wa Madinat Al Barah Zanzibar.


