

Serikali imeanzisha mashirika na taasisi za umma ili kupata ufanisi katika sekta mbalimbali na ziweze kuchangia mapato ya kuendesha shughui za Serikali na kupatikana fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na sio kuwa mzigo kwa taifa, yaani sio kufanya shughuli zake kwa hasara.