Hazina-Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Msajili wa Hazina Sanya abainisha mafanikio ikiwemo kupanda kwa gawio laserikali, asisitiza dhamira na malengo ya Rais Dk. Mwinyi lazima yatimizwe

July 27, 2024

Uwepo wa Mashirika ya Umma ni kichocheo cha maendeleo ya Uchumi”. Hii ni kauli mbiu inayotumiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar kuonyeshaumuhimu wa mashirika na taasisi za umma katika maendeleo ya nchi.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amekuwa mstari wa mbele kuchagiza mafanikio makubwa ya mashirika na taasisi za umma kutokana na maono yake.Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar inayoongozwa na Waheed Ibrahim Muhammed Sanya imemtaja Dk. Mwinyi kuwa kielelezo cha mafanikio na utendaji wa mashirika na taasisi za umma ikiwemo kuongezeka kwa gawio la serikali kwa mashirika hayo kutoka sh. bilioni 5.8 hadi sh. bilioni 13.7.