

Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wataalamu wa Udhibiti wa Ubadhirifu na Ufisadi Tanzania ( ACFE) leo tarehe 27/01/2025 wametia saini hati ya mashirikiano (MoU) yenye lengo la kushirikiana katika maeneo yafuatayo:
- Kutoa elimu kwa watendaji wa taasisi za umma katika kujua masuala ya ubadhirifu na ufisadi unaofanyika katika taasisi za umma.
- Kutoa elimu ya masuala ya kubaini, kugundua na kujiepusha na ubadhirifu na ufisadi katika mashirika ya umma.
- Kuwa na mashirikiano ya karibu katika masuala ya ukaguzi maalum na uchunguzi wa vihatarishi mbali mbali katika mashirika ya umma.
- kuanza kuwajengea uwezo maafisa wa ofisi ya Msajili Wa Hazina Zanzibar.
- Kushiriki mikutano na mafunzo ya kikanda na kimataifa kwa maafisa wa ofisi ya Msajili Wa Hazina
Mashirikiano hayo yatakuwa kwa muda wa miaka 3 na kutakuwa na kamati ya wataalamu kutoka pande zote mbili ili kusimamia na kuyafanyia kazi maeneo ya mashirikiano