Hazina-Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar

Msajili wa Hazina, Waheed Muhammad Ibrahim Sanya leo tarehe 13/03/2025 alikuwa na kikao cha pamoja na viongozi wa CEOs Forum Tanzania Bara.

Msajili wa Hazina, Waheed Muhammad Ibrahim Sanya leo tarehe 13/03/2025 alikuwa na kikao cha pamoja na viongozi wa CEOs Forum Tanzania Bara. CEOs Forum ni jumuiya inayowakutanisha watendaji wa wakuu wa mashirika ya umma Tanzania Bara kwa lengo la kuzungumza mafanikio na changamoto zinajitokeza katika Taasisi zao ili kushauriana kwa pamoja nini cha kufanya katika kufikia malengo ya Mashirika hayo na kuleta maendeleo kwa nchi. Hivyo, Msajili alikutana na viongozi hao kwa lengo la kupata uzoefu wa CEOs Forum ili Wakuu wa Mashirika ya Umma Zanzibar wawe na chombo kama hicho chenye lengo la kutatua changamoto zinazokuwa kikwazo ikiwa watendaji hao hawana sehemu ya kukutana na kuzungumza lugha mojo.Kikao hicho kilifanyika Dar es Salaam katika Ofisi za PSSSF. Aidha, katika kikao hicho mbali ya kuhudhuriwa na watendaji wakuu wa CEOs Forum, pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa ZEEA, Maafisa waandamizi kutoka Ofisi ya Msajili Zanzibar na wenyeji Mwakilishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Tanzania Bara. Baada ya majadiliano yaliyolenga kuanzisha CEOs Forum Zanzibar, kikao kiliazimia kufanya taratibu zote za kuwa na hio Forum kisheria lakini wanaweza kuanza kwa kuwakutanisha Watendaji wakuu ili walijue hili na walibebe kwa nguvu zote huku Msajili wa Hazina Zanzibar akibakia kiwa mlezi na mshauri.

Kwa niaba ya Msajili wa Hazina, Ndugu Khadija Masoud Haji Mkurugenzi Utumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina akipokea Tunzo ya shukrani kutoka kwa Uongozi wa Taasisi ya Wataalamu wa Udhibiti wa Udanganyifu katika Kongamano la Kimataifa la Mapambano dhidi ya Udanganyifu katika Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa niaba ya Msajili wa Hazina, Ndugu Khadija Masoud Haji Mkurugenzi Utumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina akipokea Tunzo ya shukrani kutoka kwa Uongozi wa Taasisi ya Wataalamu wa Udhibiti wa Udanganyifu katika Kongamano la Kimataifa la Mapambano dhidi ya Udanganyifu katika Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki. Kongamano hilo limeanza Tarehe 24-28 Februari, 2025 katika Ukumbi wa Madinat Al Barah Zanzibar.

“Azma ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni kuleta mabadiliko kwa mashirika na taasisi za umma Zanzibar”-Mhe Dkt. Saada Salum Mkuya

“Azma ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni kuleta mabadiliko kwa mashirika na taasisi za umma Zanzibar. Kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwenye Mashirika ya Umma hususan katika kutoa huduma bora kwa wananchi, kuhakikisha yanakamilisha malengo na mikakati ya Serikali iliyojiwekea.” Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na MipangoMhe Dkt. Saada Salum Mkuya

Serikali imeanzisha mashirika na taasisi za umma ili kupata ufanisi katika sekta mbalimbali na ziweze kuchangia mapato ya kuendesha shughui za Serikali na kupatikana fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na sio kuwa mzigo kwa taifa, yaani sio kufanya shughuli zake kwa hasara.

Serikali imeanzisha mashirika na taasisi za umma ili kupata ufanisi katika sekta mbalimbali na ziweze kuchangia mapato ya kuendesha shughui za Serikali na kupatikana fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na sio kuwa mzigo kwa taifa, yaani sio kufanya shughuli zake kwa hasara.

Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wataalamu wa Udhibiti wa Ubadhirifu na Ufisadi Tanzania ( ACFE) leo tarehe 27/01/2025 wametia saini hati ya mashirikiano (MoU)Mafunzo haya kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma yameandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina yakilenga kuwajengea uwezo zaidi

Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wataalamu wa Udhibiti wa Ubadhirifu na Ufisadi Tanzania ( ACFE) leo tarehe 27/01/2025 wametia saini hati ya mashirikiano (MoU) yenye lengo la kushirikiana katika maeneo yafuatayo:

Msajili wa Hazina Sanya abainisha mafanikio ikiwemo kupanda kwa gawio laserikali, asisitiza dhamira na malengo ya Rais Dk. Mwinyi lazima yatimizwe

Uwepo wa Mashirika ya Umma ni kichocheo cha maendeleo ya Uchumi”. Hii ni kauli mbiu inayotumiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar kuonyeshaumuhimu wa mashirika na taasisi za umma katika maendeleo ya nchi.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amekuwa mstari wa mbele kuchagiza mafanikio makubwa ya mashirika na taasisi za umma kutokana na maono yake.Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar inayoongozwa na Waheed Ibrahim Muhammed Sanya imemtaja Dk. Mwinyi kuwa kielelezo cha mafanikio na utendaji wa mashirika na taasisi za umma ikiwemo kuongezeka kwa gawio la serikali kwa mashirika hayo kutoka sh. bilioni 5.8 hadi sh. bilioni 13.7.